Nguvu ya mashabiki yaweka soka ya Ulaya kwenye mstari wake, mageuzi yanukia
2021-04-23 16:41:40| cri

Baada ya mashabiki na wapenzi wa soka kuonyesha nguvu yao barani ulaya na kuvunja njama ya vilabu tajiri, sasa kumekuwa na msukumo wa kufanyika kwa mageuzi ambayo yatawapa sauti ya maamuzi mashabiki wa soma. Nchini Uingereza klabu sita kubwa ambazo zilitangaza nia ya kujiunga na European Super League, zimekumbwa na wakati mgumu na upinzani mkali kutoka kwa mashabiki, ambao licha ya vizuizi vya janga la korona, waliibuka kutoka nyumbani kuandamana kupinga jaribio la matajiri kuwaibia timu zao kwa manufaa yao ya kiuchumi. Tayari kumeanza kuwa na msukumo wa kutaka kuwe na mageuzi ya utaratibu wa kusimamia umiliki, maamuzi kwenye klabu za soka za Uingereza ili kuepusha njama kama hiyo kutokea tena.