Zidane amsifu Karim Benzema kwa kuwa mchezaji mwenye nidhamu na bidii
2021-04-23 16:40:59| cri

Kocha Mkuu wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa huwa anapata tabu kupanga kikosi chake pale ambapo mshambuliaji wake Karim Benzema anakuwa hayupo katika mpango wa mchezo wake. Mshambuliaji huyo alijiunga na kikosi cha Real Madrid msimu wa 2014 rekodi zinaonyesha kwamba hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu katika michuano yote akiwa ndani ya timu hiyo. Zidane amesema kuwa nyota huyo amekuwa akionyesha kiwango bora muda wote jambo ambalo ni bora kwake na timu pia. Zidane amesema Benzema amekuwa akionyesha kiwango cha juu uwanjani, na amekuwa akiwaongoza wenzake kufanya kazi kutokana na uzoefu wake mkubwa. Amesema kuwa anakuwa na wakati mgumu anapokosekana uwanjani.