Watu wa China wasoma vitabu zaidi katika mwaka 2020
2021-04-23 20:04:04| CRI

Watu wa China wasoma vitabu zaidi katika mwaka 2020_fororder_VCG111326829899

Utafiti wa kitaifa kuhusu usomaji umeonyesha kuwa, watu wazima na watoto wamesoma vitabu vingi zaidi vya karatasi na vya digitali katika mwaka 2020 kuliko mwaka uliopita nchini China.

Utafiti huo unaonyesha kuwa, katika mwaka 2020 watu walisoma vitabu 4.7 vya karatasi na vitabu 3.29 vya dijitali kwa kila mtu. Wakati huo huo, kusoma kwenye mtandao wa Internet na kusoma kwa simu za mkononi kumekuwa njia kuu za kusoma kwa watu wazima wa mijini.