Maonesho ya biashara kufanyika Mwanza Tanzania
2021-04-23 18:38:26| cri

Zaidi ya wafanyabiashara na wadau 1,000 wa sekta ya Utalii kutoka nchini Tanzania na nje ya nchi wanatarajia kukutana mjini Mwanza katika jukwaa la biashara (Tanzania Business Summit) lengo likiwa kufanya maonesho ya biashara, utalii na uwekezaji.

Mratibu wa jukwaa hilo, Bernad Mwata amesema maonesho hayo yatafanyika Rock City Mall kwa siku tatu kuanzia  Aprili 30 hadi Mei 2 mwaka huu  na yatahusisha nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Burudi, Uganda, Rwanda na Afrika ya Kusini.

Amesema tamasha hilo makakati mkubwa ni kuwaunganisha wafanyabiashara kutoka mkoani Mwanza na maeneo mengine mbalimbali hivyo kupitia jukwaa hilo wafanyabiashara watabadilishana mawazo pamoja na kufanya utatuzi wa changamoto zinazowakabili.

Amesema lengo la maonesho haya ni kutangaza biashara na utalii kwa ajili ya kuwainua wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi hivyobaadhi ya washiriki ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT),  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), Idara ya Utalii.