Rais wa Iran azindua miradi ya kilimo na kusema vikwazo havitaizuia Iran
2021-04-23 08:39:22| CRI

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema vikwazo haviwezi kuizuia Iran kujiendeleza, wakati alipozindua miradi 4,635 ya kilimo kote nchini kwenye hafla iliyofanyika kwa njia ya mtandao.

Rais Rouhani amesema moja ya malengo ya kuzindua miradi hiyo mikubwa ni kuifanya dunia ielewe kwamba vikwazo na shinikizo haviwezi kuizuia Iran kutimiza maendeleo.