Wanaharakati wa Afrika wazitaka nchi tajiri kuchangia kwa haki kwenye makubaliano kuhusu tabianchi
2021-04-23 09:06:09| CRI

Wanaharakati wa mambo ya tabia nchi barani Afrika wamesema nchi zilizoendelea zinawajibika zaidi kwa utoaji wa hewa ya ukaa, kwa hiyo zinatakiwa kuheshimu ahadi ya kutoa fedha kwa lengo la kuimarisha mwitikio wa msukosuko wa tabia nchi barani Afrika.

Mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la Afrika kuhusu haki ya hali ya hewa Bw. Mithika Mwenda, amesema uongozi kutoka nchi zilizoendelea ni muhimu katika kuhimiza uwezo wa nchi za Afrika kuzoea mabadiliko ya tabia nchi.

Bw. Mwenda ametoa mwito kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi kuwa nchi zilizoendelea ziongeze viwango vya kupunguza hewa ya ukaa, ziheshimu ahadi ya kuchangia fedha kwenye mfuko wa maendeleo bila uchafuzi na kuhimiza mpango wa ufufuaji wa uchumi wenye haki na usawa baada ya janga la COVID-19.