Maonesho ya Kimataifa ya bidhaa za matumizi ya China yafunguliwa
2021-05-07 18:58:12| CRI

Maonesho ya Kimataifa ya bidhaa za matumizi ya China yafunguliwa_fororder_VCG111328879910

Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa za matumizi ya China yamefunguliwa jana mjini Haikou, mkoani Hainan. Maonesho hayo yametoa jukwaa la kuonyesha na kufanya biashara ya bidhaa za matumizi zenye sifa ya juu duniani, na kampuni zaidi 1500 za ndani na nje ya China zimeshiriki kwenye maonesho hayo. Kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo, wadau wa nchi mbalimbali wameeleza matarajio ya kuzidisha ushirikiano na China, na kunufaisha fursa katika soko la China.

Katika salamu zake za ufunguzi wa maonyesho hayo alizozitoa kwa njia ya video, Waziri mkuu wa Thailand Prayuth Chan-ocha amesema, sera ya bandari ya biashara ya huria ya Hainan na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” zinaendana na maslahi ya Thailand na China, pia zitasaidia uchumi wa nchi hizo mbili kufufuka na kuendelea zaidi.

“Ninafurahi kusikia idara ya biashara ya kimataifa ya Thailand na idara ya biashara ya Hainan zinapanga kusaini makubaliano, ili kuhimiza ushirikiano wa kibiashara, hususan ushirikiano kati ya makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati, ushirikiano wa biashara ya kielektroniki ya kuvuka mipaka, na kuungana kibiashara. Natumai makubaliano hayo yatapanua zaidi sekta za ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Thailand na Hainan. ”

Maonesho ya Kimataifa ya bidhaa za matumizi ya China yafunguliwa_fororder_VCG111328879913

Uswiss ni nchi mgeni wa heshima wa maonyesho hayo, bidhaa na huduma mpya za makampuni zaidi 20 kutoka Uswiss zitaonyeshwa kwenye jumba la Uswiss. Balozi wa Uswiss nchini China Bernardino Regazzoni amesoma barua za pongezi kutoka Kansella wa Uswiss Guy Parmelin, akisema anafurahi nchi yake kuchaguliwa kuwa nchi mgeni wa heshima.

“Mwaliko huu umeonyesha uhusiano wenye sifa ya juu kwenye msingi wa kuaminiana kati ya Uswisi na China. Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeimarika kupitia mazungumzo na ushirikiano, pia zimeimarisha maelewano katika sekta mbalimbali. ”

Maonyesho hayo yana maeneo tano ya maisha ya mtindo wa kisasa, mapambo ya vito, vyakula vya ngazi ya juu na vyakula vya afya, maisha ya utalii na matumizi ya huduma.