WHO: China yanufaika na matokeo mazuri ya udhibiti wenye ufanisi wa maambukizi ya COVID-19
2021-05-11 18:33:29| CRI

WHO: China yanufaika na matokeo mazuri ya udhibiti wenye ufanisi wa maambukizi ya COVID-19_fororder_瑞安

Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani WHO jana wamesema, mji wa Wuhan na sehemu nyingi nchini China zinanufaika na matokeo mazuri ya udhibiti wenye ufanisi wa maambukizi ya COVID-19, hali inayoonyesha kwamba watu wana machaguo mengi zaidi katika maisha ya jamii na uchumi baada ya maambukizi ya COVID-19 kuwa katika kiwango cha chini.

Mkurugenzi wa miradi ya dharura ya afya wa WHO Michael Ryan amesema, nchi zinazochukua hatua kamili za udhibiti wa janga la COVID-19, zinaposhughulikia masuala yote pia zinazingatia kuendelea kupunguza mawasiliano kati ya watu wa kawaida na watu wanaoambukizwa virusi vya Corona, hivyo kupunguza kasi ya maambukizi na kuwa ya kiwango cha chini zaidi.

Hata hivyo Bw. Ryan anaamini kuwa China na nchi nyingine zenye kiasi cha chini cha maambukizi ya COVID-19 zitaendelea kuchukua tahadhari ili kudumisha kiwango cha sasa cha kinga na udhibiti wa janga la COVID-19.