Kampuni ya Huawei yazindua mradi wa ajira kwa wahitimu nchini Kenya
2021-05-13 20:06:00| Cri

Kampuni ya Huawei yazindua mradi wa ajira kwa wahitimu nchini Kenya_fororder_VCG111329562765

Kampuni ya Teknolojia za Mawasiliano ya Simu ya China, Huawei, imetangaza kuzindua mradi utakaowezesha wahitimu wa vyuo vikuu nchini Kenya kupata ajira na mafunzo wakiwa kazini.

Fursa zaidi ya 30 za ajira na mafunzo kazini zitapatikana kwa vijana nchini humo waliosomea teknolojia ya mawasiliano (ICT) chini ya program inayoungwa mkono na moja ya kampuni kubwa za huduma ya simu ya China Telecom.

Katibu mkuu wa Wizara ya Teknolojia ya Mawasiliano, Uvumbuzi na Masuala ya Vijana nchini Kenya, Joe Mucheru, amesifu uratibu wa Huawei katika kuboresha uwezo wa kidijitali kwa vijana nchini Kenya na kuharakisha kutimizwa kwa lengo la nchi hiyo la kuwa taifa lenye uelewa mkubwa wa kiuchumi.