Kenya-Faida ya Safaricom inaweza kushuka kwa mara ya kwanza kutokana na kipigo cha Covid-19
2021-05-13 18:56:45| cri

Kampuni yenye faida kubwa zaidi nchini Kenya, Safaricom ,inaweza kuandikisha kupungua kwa mapato ya mwaka mzima kutokana na athari za Covid-19, hii ikiwa ni mara ya kwanza katika zaidi ya miongo miwili ya shughuli zake.

Mwaka wa kifedha wa kampuni hiyo ya mawasiliano chini ya ukaguzi uligubikwa na usumbufu wa kiuchumi kutokana na janga la Covid-19, na kukwamisha mifumo ya matumizi ya watumiaji.

Kipindi cha kuripoti kilianza Mwezi Machi mwaka jana wakati Kenya iliripoti kesi yake ya kwanza ya Covid-19.

Faida ya nusu mwaka ya kampuni ya Safaricom ilishuka kwa asilimia sita hadi Sh33 bilioni ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2020 ikihusishwa na ukadiriaji wa sifuri wa miamala ya M-Pesa na kushuka kwa mapato ya sauti kutokana na watumiaji kukata bajeti ya mawasiliano kutokana na shinikizo la kiuchumi la Covid-19.

M-Pesa ndio ilyoathirika zaidi, ikiandikisha kushuka kwa mwaka hadi mwaka kwa asilimia 14.5.

Huduma hiyo ilichangia Sh35.9 bilioni kwa mapato ya kampuni ikilinganishwa na Sh42 bilioni zilizorekodiwa kwa kipindi kama hicho katika mwaka uliopita wa fedha.