Rais Putin amesema Russia inaunga mkono Umoja wa mataifa
2021-05-14 09:18:04| CRI

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema Russia inaunga mkono nafasi ya Umoja wa mataifa kwenye utatuzi wa maswala ya kimataifa.

Akiongea kwa njia ya video na Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ambaye yuko ziarani mjini Moscow, Rais Putin amethibitisha kuwa Russia itaendelea kushirikiana na Umoja wa mataifa na mashirika yake maalum kwenye utoaji wa chanjo na kutoa matibabu kwenye magonjwa mbalimbali.

Kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Israel na Palestina, Rais Putin na Bw. Guterres wamezitaka pande zote mbili kukomesha matumizi ya mabavu na kuhakikisha usalama wa raia.

Viongozi hao pia wamejadili mambo ya nchi za mashariki ya kati kama vile Syria, Libya, Yemen na Afghanistan, pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.