NDONDI: Anthony Joshua na Tyson Fury kuzichapa Agosti 14
2021-05-14 17:00:27| cri

Pambano la ngumi kati ya mabondia wawili waingereza Anthony Joshua na Tyson Fury litafanyika Agosti 14 mwaka huu huko Saudia Arabia, kwenye uwanja maalumu utakaojengwa mahususi kwa pambano hilo. Promota wa AJ Eddie Hearn amethibitisha kuwa makubaliano ya pambano hilo yamefikiwa, ingawa bado upande wa bondia Tyson Fury haujathibitisha kufikia makubaliano ya kufanyika kwa pambano hilo. Pambano hili linatajwa kuwa ni pambano kubwa katika historia ya mchezo wa masumbwi Uingereza, kutokana na ubora wa mabondia wote ikiwemo kushikilia mikando yote ya uzani wa juu. Anthony Joshua anashikilia mikanda minne ya uzito wa juu ambayo ni IBF, WBA , IBO na WBO na Tyson Fury anashikilia mkanda wa WBC.