Wahamiaji haramu zaidi ya 150 warudishwa Libya
2021-05-14 17:09:30| cri

Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) limesema, wahamiaji haramu zaidi ya 150 wamezuiliwa na kurudishwa Libya.

Shirika hilo pia limesema, wahamiaji 17 wamekufa maji katika pwani ya Tunisia, ikiwa ni siku mbili baada ya kuondoka Libya.

Shirika hilo limesema, tangu mwaka huu uanze, zaidi ya wahamiaji elfu 7 haramu wamezuiliwa na kurejeshwa Libya, huku mamia wengine wamefariki ama hawajulikani walipo wakiwa safarini kupitia bahari ya Mediteranean.