Israel yasema itaendeleza mashambulizi ya kijeshi katika ukanda wa Gaza
2021-05-14 08:59:16| CRI

Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amesema Israel itaendeleza mashambulizi ya kijeshi kwenye ukanda wa Gaza.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, inasema Bw. Netanyahu siku hiyo alizungumza kwa njia ya simu na rais Joe Biden wa Marekani kuhusu hali ya sasa kati ya Israel na Palestina, na kusema Israel itaendeleza operesheni za kijeshi dhidi ya kundi la Hamas na makundi mengine yenye silaha kwenye ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel siku hiyo limesema linafanya maandalizi ya kuanza mashambulizi ya ardhini kwenye ukanda huo.