Kenya kuifanyia mageuzi sekta ya chai ili kuongeza upatikanaji
2021-05-14 20:08:55| CRI

Kenya kuifanyia mageuzi sekta ya chai ili kuongeza upatikanaji_fororder_肯尼亚 茶叶

Wizara ya Kilimo nchini Kenya imerejea tena ahadi yake ya kuifanyia marekebisho sekta ya chai ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka duniani.

Waziri wa Wizara hiyo Peter Munya ameliambia jukwaa la mageuzi ya sekta ya chai jijini Nairobi kuwa, mageuzi hayo yanafanywa ili kusaidia kuleta nguvu mpya kwenye sekta hiyo ambayo imekuwa ikishuka katika miaka michache iliyopita.

Amesema uongozi mbaya katika sekta hiyo, hususan katika kampuni ndogo za utengenezaji wa chai, umeboreka kutokana na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya. Pia amesema, chai zote zinazozalishwa Kenya kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi zitauzwa kwa njia maalum ya mnada mara mageuzi hayo yatakapoanza kutekelezwa.