Watu tisa wauawa kwenye mashambulizi katika sikukuu ya Eid nchini Afghanistan
2021-05-14 08:58:42| CRI

Mashambulizi yaliyotokea jana Alhamisi ambayo ni sikukuu ya Eid ya waislam nchini Afghanistan yamesababisha vifo vya raia tisa.

Rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo jana alitoa wito kwa kundi la Taliban kuacha mapambano na mashambulizi, na kuunga mkono mchakato wa amani, ili kutafuta ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo.

Kabla ya hapo, kundi la Taliban na jeshi la serikali walitangaza kusitisha mapambano kwa siku tatu kwa ajili ya sikukuu ya Eid.