Mke atoa ombi la talaka baada ya kugundua kuwa mume ana saratani
2021-05-14 10:33:12| Cri

Siku hizi wanandoa wanaweza kuchagua kutalikiana kama hawapendeani. Lakini katika “Sheria ya zamani ya ndoa, kulikuwa na hali moja tu ambayo ndoa inaweza kufutwa, ambayo ni kuwa watu wanafunga ndoa kutokana na hali ya kulazimiswa, na kwenye sheria mpya ya mambo ya kiraia, imewekwa hali nyingine ya kufutwa kwa ndoa: yaani kama upande mmoja wa wanandoa una ugonjwa mbaya, na haukuweka wazi ukweli huo, upande mwingine unaweza kutoa ombi mahakamani kufuta ndoa.

Muda si mrefu uliopita, mahakama ya Haimen ya mji wa Nantong ilisikiliza kesi kama hii. Xiaolin na Xiaozhang walioana baada ya kufahamiana kwa mwaka mmoja, na uhusiano wao ni mzuri sana. Lakini katika usiku wa karamu ya harusi, bibi harusi Xiao Zhang aligundua kuwa Xiao Lin alikuwa na mwenendo wa  ajabu.

Mwanzoni Xiao Lin alikanusha, akisema alikuwa anakula tu vitu vya kujenga afya. Baada ya kuendelea kuulizwa, alimwambia Xiao Zhang ukweli wa mambo, akisema alipatwa saratani ya tezi(thyroid gland) miaka mingi iliyopita, lakini sasa amepona, analohitaji kufanya ni kutumia dawa kwa muda mrefu, na haitadhuru maisha na kazi, pamoja na uzazi.

 

Lakini Xiao Zhang anaamini kuwa mume wake alikusudia kuficha hali ya ugonjwa kabla ya ndoa, na akimnyima haki yake ya kuchagua ndoa, kwa hivyo alitoa mashtaka mahakamani na kutaka ndoa hiyo ifutwe. Na kama ugonjwa huu unahusishwa katika “magonjwa makali” ambayo yatafanya ndoa kufutwa ni tatizo kubwa kwa kesi hiyo. Sheria ya mambo ya kiraia haijafafanua “magonjwa makali”, kwa hiyo kwa kawaida mahakama inatoa uamuzi kwa kufuata sheria na kanuni zikiwemo “Sheria ya Afya ya Mama na Watoto”.

Kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Mama na Watoto, hali hii ya Xiao Lin hautambuliwi kuwa ni “ugonjwa mkubwa” kutokana kuwa umepona vizuri baada upasuaji. Mwishowe mahakama ilikataa ombi la Xiao Zhang la kufuta ndoa.