Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya mfanyakazi wa misaada nchini Sudan Kusini
2021-05-14 09:34:51| cri

 

 

Mratibu wa mambo ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Bw. Alain Noudehou amelaani mauaji ya mfanyakazi wa misaada kwenye kaunti ya Budi mkoani Ikweta ya Mashariki, Sudan Kusini.

Bw. Noudehou amesema mfanyakazi mmoja aliuawa jumatano wakati wahalifu walipofyatulia risasi gari la misaada ya kibinadamu lililokuwa likisafiri kwenda kwenye kituo cha afya.

Bw. Noudehou amezitaka serikali na jamii za Sudan Kusini zihakikishe wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanaweza kupita salama barabarani na kutoa msaada kwa watu waishio katika mazingira magumu nchini humo.