SOKA: Man City na Chelsea kuoneshana kazi nchini Ureno
2021-05-14 17:00:47| cri

Shirikisho la soka Barani Ulaya (UEFA) limethibitisha kwamba Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Chelsea na Manchester City, sasa itachezwa mjini Porto nchini Ureno katika Dimba la Dragao Mei 29 mwaka huu. UEFA ilitaka fainali kuchezwa Wembley nchini Uingereza, lakini kulikuwa na hatua za kuzingatia juu ya kuondoa sheria za karantini kwa wafanyikazi 2,000, wafadhili, VIP na Vyombo vya Habari vya kigeni vitakavyoenda nchini humo. Ni mashabiki 12,000 tu, 6,000 kutoka kila kikosi ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mtanange huo moja kwa moja.