Whatsapp kuanza kutekeleza masharti mapya wiki hii
2021-05-14 17:04:47| cri

Mtandao wa kijamii wa WhatsApp hivi sasa umeanza kuongeza masharti zaidi kwa mtandao wake kwa ajili ya kuboresha biashara. Sheria na mikakati hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumamosi wiki hii.

Tangazo hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara kwenye skrini mtumizi anapoingia kwenye mtandao wa WhatsApp.

Mtandao huo hata hivyo umehakikishia watumizi jumbe zao zitakuwa salama licha ya mabadiliko hayo.

Mtandao huo umesema hauwezi kasoma wala kuskiza jumbe za kibinafsi za wateja kwa sababu ni kinyume na kanuni za sharia za kampuni.