Afrika CDC: Nchi za Afrika zimepata dozi milioni 38 za chanjo ya COVID-19
2021-05-14 09:17:18| CRI

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Maradhi cha Afrika (Africa CDC) kimesema hadi sasa nchi za Afrika zimepata dozi milioni 38.03 za chanjo ya COVID-19.

Kituo hicho kimesema dozi milioni 22.4 kati ya milioni 38.03 tayari zimetolewa, kiasi ambacho ni asilimia 1.48 kwa bara zima la Afrika, na idadi ya watu waliopatiwa chanjo kikamilifu ni asilimia 0.40.

Hadi sasa nchi za Afrika zimetumia asilimia 58.87 ya chanjo waliyopewa, huku Morocco, Nigeria, Ethiopia, Misri na Kenya zikiwa ni nchi zilizotoa chanjo hiyo kwa wingi zaidi.

Morocco ndio imetoa chanjo kwa kiwango cha juu zaidi kwa kuchanja asilimia 11.9 ya watu wake wote, Nigeria ni ya pili ikiwa imechanja asilimia 0.82 ya watu wake wote.

Na hadi kufikia jana watu milioni 4.6 walikuwa wameambukizwa COVID-19 barani Afrika na watu laki 1.25 wamepoteza maisha yao.