China yahimiza Marekani kutambua kuwa maisha ya Waislamu wa Palestina yana thamani
2021-05-14 19:40:14| CRI

China yahimiza Marekani kutambua kuwa maisha ya Waislamu wa Palestina yana thamani_fororder_VCG111329866530

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, Marekani inalizuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa taarifa kuhusu hali ya Palestina na Israel, na kusema Marekani inapaswa kutambua kuwa maisha ya Waislamu wa Palestina pia yana thamani.

Bi. Hua amesema, Marekani inatetea kuzingatia haki za binadamu za Waislamu, lakini kwa sasa nchi hiyo haifuatilii usalama wa Wailsamu nchini Palestina wanaokabiliwa na mgogoro mpya kati ya nchi hiyo na Israel.

Amesema nchi wanachama wa Baraza la Usalama wanafuatilia sana mgogoro kati ya Palestina na Israel, na kulitaka Baraza hilo kuchukua nafasi yake kuhimiza hali hiyo kutulia. Lakini Marekani inapinga mwenyekiti wa Baraza hilo kutoa taarifa katika mikutano miwili ya dharura iliyofanyika tarehe 10 na tarehe 12 mwezi huu.