Mashindano ya video na picha ya China na Afrika yazinduliwa
2021-05-21 19:55:17| CRI

Mashindano ya video na picha ya China na Afrika yazinduliwa_fororder_VCG41513969720

Mashindano ya video na picha ya China na Afrika kwa mwaka 2021 yamezinduliwa rasmi leo mjini Nairobi.

Mashindano hayo yamefadhiliwa kwa pamoja na sekretarieti ya ufuatiliaji ya China ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na Shirika la Uchapishaji la China, kwa lengo la kuimarisha maelewano kati ya Wachina na Waafrika.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuzingatia urafiki, na mustakabali kwa pamoja”. Ukusanyaji wa kazi kwa ajili ya shindano hilo unaaza tarehe 21 Mei hadi tarehe 20 Julai, na kazi ya kuchagua washindi itaanza tarehe 1 Agosti, na kuendelea hadi mwezi Septemba. Washiriki watakuwa ni watu na taasisi za China na Afrika