Uganda yaanza kipindi cha pili cha udungaji wa chanjo ya COVID-19
2021-05-21 19:49:06| CRI

Uganda yaanza kipindi cha pili cha udungaji wa chanjo ya COVID-19_fororder_VCG31N1306322406

Uganda leo imeanza kipindi cha pili cha zoezi la udungaji wa chanjo ya COVID-19.

Waziri wa afya wa nchi hiyo Bibi Ruth Aceng, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Sam Kutesa na mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Uganda Yonas Tegegn Woldemariam wamekuwa miongoni mwa watu waliopata dozi ya pili ya chanjo ya Astrazeneca katika makao makuu ya wizara ya Afya mjini Kampala.

Waziri wa afya Bibi Ruth Aceng amesema wizara yake inapendekeza watu wote waliodungwa dozi ya kwanza na kukamilisha wiki 8 kwenda kituo cha karibu cha utoaji wa chanjo kupata dozi ya pili. Amesema chanjo ni salama na yenye ufanisi.

Tarehe 10 Machi Uganda ilianza kipindi cha kwanza cha zoezi la udungaji wa chanjo kwa walio kwenye hatari kubwa zaidi, wakiwemo wafanyakazi wa afya, walimu, wafanyakazi wa kijamii, walinzi, wakuu na wale wenye magonjwa ya kimsingi.