China yarusha chombo kilichobeba wanaanga kwenda kwenye ujenzi wa kituo chake cha anga za mbali
2021-06-17 10:24:31| Cri

China leo Alhamis imerusha chombo cha Shenzhou-12 kilichobeba wanaanga watatu, ambacho kinatarajiwa kuwapeleka kwenye kituo chake cha anga ya mbali cha Tianhe kwa kazi ya miezi mitatu.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga za Mbali la China, chombo hicho kilichobebwa na roketi ya Long March-2F, kilirushwa kwenye kituo cha kurushia cha Jiuquan, kilichopo kwenye jangwa la Gobi kaskazini magharibi mwa China. Hii ni safari ya saba ya China kupeleka wanaanga kwenye anga za mbali, na ya kwanza katika kipindi cha ujenzi wa kituo cha anga za mbali cha China. Pia ni ya kwanza kwa karibu miaka mitano tangu safari ya mwisho ya anga za mbali ya China