Vyombo vya habari vya nchi za magharibi vyahimizwa kuacha ubaguzi dhidi ya Chama cha Kikomunisti cha China
2021-06-23 09:44:30| Cri

Balozi wa Afrika Kusini nchini China Siyabonga Cwele amesema, vyombo vya habari vya nchi za magharibi vinapaswa kuacha ubaguzi dhidi ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na kufanya uchunguzi halisi nchini China, ili kutoa ripoti kuhusu Chama hicho kwa kufuata hali halisi.

Balozi Siyabonga amesema, Chama kicho kimeendelea kujijenga na kujiimarisha, ili kutimiza malengo ya maendeleo kiliyoahidi kwa wananchi wa nchi hiyo, pia kimeonesha uwezo mkubwa wa kushikamana na watu wa hali tofauti.

Balozi Siyabonga amesisitiza kuwa, kila nchi ina haki ya kuchagua njia yake ya kujiendeleza, ambayo haiwezi kuzuiwa kwa kisingizio chochote.