Mbio za magari za Safari Rally kuchochea ukuaji wa biashara Naivasha
2021-06-24 14:37:58| cri

 

 

Hoteli katika kaunti ndogo ya Naivasha zimejaa huku mamia ya wageni wakiendelea kumiminika kwenye kaunti hiyo, wakisubiri kushuhudia mashindano ya Mbio za Magari Duniani WRC yatakayofanyika wiki hii.

Waandaaji wa mashindano hayo wamesema watu wasiopungua elfu kumi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria mashindano hayo.

Ofisa mtendaji mkuu wa Mbio za Magari Duniani WRC Phineas Kimathi amesema, mashindano hayo maarufu ambayo yatatangazwa moja kwa moja na vituo 155 vya televisheni kote duniani, yatachochea ukuaji wa biashara nchini Kenya.