Polisi nchini Kenya wamuua mtuhumiwa wa ugaidi katika eneo la pwani
2021-06-24 09:19:23| Cri

Kamanda wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Pwani (DCI) nchini Kenya, Bw. Njiru amesema polisi wa idara ya kupambana na ugaidi wamemuua kwa kumpiga risasi mtuhumiwa wa ugaidi katika Kaunti ya Kwale mkoani humo.

Inadaiwa kuwa, mshukiwa huyo wa ugaidi alipanga kushambulia kituo cha usalama na kuiba silaha katika eneo hilo.

Njiru ameongeza kuwa washukiwa wengine wawili walitoroka na majeraha ya risasi.