Uganda Airlines lasitisha mkataba wa mafuta na MixJet Flight Support.
2021-07-20 07:56:07| CRI

Huenda shirika la ndege la Uganda likasitisha mkataba wake na kampuni ya MixJet Flight Support, yenye makao yake Dubai. MixJet imekuwa ikisambazia ndege za Uganda mafuta kwa muda mrefu. Hata hivyo, kufuatia visa viwili vya hivi punde katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo abiria walicheleweshwa kwa zaidi ya saa moja kwa sababu ya mafuta ya ndege kucheleweshwa, shirika la ndege la Uganda huenda likachukuwa hatua hii ya kusitisha mkataba na MixJet.

Swala hili liliibua mdahalo mkali kwenye mitandao ya kijamii, na kuulazimu usimamizi wa shirika la Uganda Airlines kutoa taarifa rasmi kuhusu matukio haya mawili. Kulingana na abiria, walikuwa na mtazamo kwamba huenda ndege hizi za Uganda Airlines ziliishiwa mafuta zikiwa safarini, jambo ambalo usimamizi wa shirika hilo ulipinga vikali.