Kenya: Sasa Itakubidi Ulipe Ili Kutumia Zoom nchini Kenya
2021-07-21 07:44:57| CRI

Biashara zitatozwa kwa kutumia Zoom nchini Kenya, kampuni hiyo imetangaza.

Programu ya mkutano wa video inasema imelazimika kupitisha malipo kwa watumiaji wake baada ya serikali kuweka Ushuru kwenye huduma hiyo.

Kupitia barua pepe iliyotumwa kwa wateja wake nchini Kenya, kampuni hiyo ilisema Wakenya wataanza kulipa "mnamo au muda mfupi baada ya Agosti 1, 2021"

Hii itaathiri mashirika kwa kuwa ndio ambao kawaida hulipa huduma za Zoom.

Wakati watumiaji wengi wa Zoom hutumia mpango wa kimsingi, ambao ni bure, biashara nyingi kubwa kati ya mashirika mengine na mashirika ya serikali hulipa kati ya Sh15,000 ($ 150) na Sh25,000 ($ 240) kwa leseni.

Zoom imepata umaarufu tangu mwanzo wa janga la Covid-19, na kuwa programu ya mkutano wa video inayotumika zaidi ulimwenguni.

Utozwaji wa Ushuru kwa wauzaji katika jukwaa la kidijitali nchini ulianza kutumika Januari 2, mwaka huu, hatua ambayo itaona KRA ikiongeza mkusanyiko wake wa mapato.

Zoom sasa inajiunga na Facebook na YouTube ili kutoa kodi.