Serikali kulipa fidia ya Sh14 Bilioni Kwa Walioshambuliwa Na Wanyamapori Kenya
2021-07-26 07:33:15| cri

Waziri wa Utalii wa Kenya Bw Najib Balala amehimiza Shirika la Wanyamapori (KWS), kujenga uhusiano mwema na jamii kwa kuihamasisha jinsi ya kuepuka mashambulizi kutoka kwa wanyamapori.

Balala amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza mizozo kati ya binadamu na wakazi, ambapo visa hivyo vimesababisha vifo na majeraha.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitatu, serikali imetumia takriban Sh2 bilioni kulipa fidia kwa wananchi walioashambuliwa na wanyamapori nchini. Bw Balala alisema jumla ya fedha zinazostahili kulipwa wananchi walioathirika kutokana na mashambulizi ya wanyama ni Sh14 billioni. Aliongeza kuwa watu wanaoishi karibu na wanyama pori wanatakiwa kuwa waangalifu.