Wakulima Tanzania watakiwa kupunguza gharama
2021-07-26 07:33:42| cri

Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU), wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwapunguzia gharama ya uzalishaji wakulima ili kuendana na kipato chao.

Hivi sasa chuo hicho kinatekeleza mradi wa pamoja wa kupunguza umaskini kwa wakulima wadogo mkoani morogoro.

Wanafunzi hao wanaosoma kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto ya usafiri iliyosabishwa na ugonjwa wa corona, walitoa rai hiyo baada ya kufanya ziara ya mafunzo kwa vitendo katika vijiji mbalimbali vinavyotekeleza mradi huo mkoani hapa.

Ziara hiyo ililenga kuangalia namna chuo hicho kinavyotekeleza miradi mbalimbali hasa ya kilimo cha mahindi katika kusaidi kuwapunguzia wakulima umaskini kwa utoaji mafunzo ya uzalishaji wa mazao kwa tija.

Wanafunzi hao wameongeza kuwa licha ya mradi huo kuwanufaisha wakulima wengi baada ya kupata elimu ya kilimo cha kisasa, kuna haja ya wataalam kuangalia namna bora ya kuwapunguzia gharama za uzalishaji.