EAC: Benki kubwa zaid ya Misri, kununua benki kadhaa za Afrika Mashariki
2021-07-27 07:44:09| cri

Benki kubwa zaidi kwa umiliki wa  mali nchini Misri, Commercial International Bank (CIB), ina mipango ya kununua benki kadhaa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, ili kuongeza nguvu uwepo wake katika ukanda huu. CIB inasema kuwa, kupitia hatua hii, itawezesha wawekezaji kutoka Misri kupata mitaji ili wawekeza Afrika Mashariki. Mataifa ya Afrika Mashariki yanawavutia wawekezaji wengi sana kutokana na fursa nyingi zilizopo, hali kadhali, ukuaji wa eneo hili kiuchumi.

Benki hii ya Misri inayomiliki mali yenye zaidi ya thamani ya dola bilioni 27.24, ilinunua hisa asilimia 51 za Kenya Mayfair Bank, huu ukionekana kuwa mwamko mpya wa ujio wa CIB katika mataifa ya Afrika Mashariki.