Zanzibar: Utalii wazidi kuimarika
2021-07-27 07:44:58| cri

Licha ya dunia kukabiliwa na janga la corona, idadi ya watalii walioingia Zanzibara mwezi Juni mwaka huu, imeongezeka na kufikia 20,416, ikilinganishwa na 9,280 waliongia mwezi Machi mwaka huu.

Akitoa takwimu za uingiaji wa wageni kwa waandishi wa habari wikendi iliyopita, Mkuu wa Takwimu za Kiuchumi kutoka ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Abdulrauf Ramadhani Abeid, alisema Ufaransa inaongoza kwa kuleta watalii wengi Zanzibar.

Alisema wageni 11,588 waliongia nchini, ni kutoka Ulaya, ambao ni sawa na asilimia 56.8. Alisema kwa mwezi huo, Ufaransa iliongoza kwa kuleta wageni 2,232 sawa na asilimia 10.9 ya wageni wote ikifuatiwa na Poland 2,101 sawa na asilimia 10.3.

Wageni waliongia Zanzibar kwa kutumia usafiri wa boti kupitia Bandari  ya Malindi, alisema walikuwa 5,152 sawa na asilimia 25.2.  Waliongia kupitia viwanja vya ndege ni 15,264 sawa na asilimia 74.8.