Makundi 10 Ya Wafanyabiashara Thika Yapokea Mkopo Wa Sh1.4 Milioni
2021-08-11 07:52:04| CRI

VIKUNDI 10 vya wafanyabiashara vimenufaika na mkopo ya Sh1.4 milioni ili kujiendeleza zaidi.

Fedha hizo zimetolewa na serikali kupitia kwa hazina ya kuondoa ufukara yaani Poverty Eradication Fund ili kuwapa mwelekeo wa kujiendeleza kibiashara.

Afisa wa idara ya Shirika la maendeleo kaunti ndogo ya Thika Magharibi, Bi Mercy Kinoti, alieleza kuwa kila kikundi kinajumuisha kati ya watu 10 na 20 ambao wanatarajia kuendesha biashara zao kwa pamoja.

Amesema vikundi hivyo vilipokea kati ya Sh50,000 hadi Sh250,000 ili kupanua biashara zao mashinani.

Wanufaika walishauriwa kurejesha hela hizo chini ya kipindi cha miezi 12 ili pia vikundi vingine viweze kunufaika na mkopo huo.

Wote waliopokea mkopo huo walishauriwa kutumia fedha hizo kwa makini ili ziweze kuwanufaisha pamoja na familia zao.