Serikali Haijaruhusu Uagizaji Wa Chakula Chochote Cha GMO – Munya
2021-08-12 07:55:51| CRI

WAZIRI wa Kilimo Peter Munya amesisitiza kwamba serikali haijaruhusun uagizaji wa chakula kilichotengenezwa kiteknolojia (GMO) kutoka nje ya nchi.

Bw Munya amesema ukuzaji wa pamba ya GMO ndio pekee umekubalika.

Serikali ilitoa idhini ya ukuzaji wa mimea hiyo 2018, baada ya majaribirio kufanyika maeneo ya Katumani, Perkerra katika Kaunti ya Baringo, Mwea, Bura Tana na Kampi ya mawe Makueni.

Waziri amesema hayo kufuatia mswada unaoandaliwa kujadiliwa bungeni, kuruhusu au kukataa uagizaji wa chakula cha GMO.

Aidha amesema wizara yake inaendelea kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo na ambayo yanalenga kuimarisha usalama wa mazao, bidhaa za kula nchini na uchumi wa nchi.