Bei ya mafuta Kenya kutoongezwa
2021-08-16 07:38:23| cri

Mamlaka ya kudhibti bei ya mafuta nchini Kenya Epra imekanusha taarifa zinazosambazwa kuhusu kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini Kenya.Kwenye taarifa yake, Epra imesema bei ya sasa itaendelea kwa muda wa mwezi mmoja. Hatua hiyo ya serikali imepongezwa na wafanya biashara wakisema itawawezesha kutoa huduma bora kwa raia wa Kenya. Awali kumekuwa na tishio kuwa huenda serikali ikaongezeka bei ya bidhaa za mafuta jambo ambalo limepelekea baadhi ya wafanya biashara kuwa na wasiwasi.  Wazalishaji bidhaa wanasema kuna haja ya serikali ya Kenya kufanya mikutano ya mara kwa mara kuona ni jinsi gani tatizo la kupanda mara kwa mara kwa bei ya mafuta litatatuliwa.