Kenya na Uganda kujadili jinsi ya kuondoa vikwazo vya kibiashara
2021-08-30 08:04:40| CRI

Maonesho ya kibiashara kati ya Kenya na Uganda yanayotarajiwa kufanyika kati ya Septemba 8- 9 yatatilia mkazo zaidi jinsi ya kuondoa vikwazo kati ya nchi hizo mbili. Wizara ya mambo ya nje ya Uganda imesema jukwaa hilo litalenga kutafuta suluhisho la kudumu na jinsi ya kufanikisha malengo ya nchi hizo kwenye biashara. Maonesho hayo yatafanyika mjini Mombasa nchini Kenya na yatawaleta pamoja wadau katika sekta ya kilimo kutoka nchi zote mbili ambao wataonyesha bidhaa zao na kujadili jinsi ya kuweka uataratibu mzuri wa kusafirisha bidhaa nje.

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda John Mulimba amesema Kenya ni mshirika mkubwa wa Kibiashara wan chi hiyo na bidhaa nyingi za bidhaa zao ni za kilimo. Kilimo kimesalia kuwa kitega uchumi kikuu nchini Uganda ikiwa ni asilimia 24 ya pato la taifa. Biashara kati ya Kenya na Uganda imekuwa ikiimarika kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa mwaka wa 2019. Miongoni mwa bidhaa za Uganda ambazo zimepata soko kubwa nchini Kenya ni pamoja na mahindi, vyakula vya mifugo, maziwa na sukari.