Kenya kufanya juhudi kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs
2021-09-21 09:27:35| CRI

Kenya kufanya juhudi kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs_fororder_VCG111349123912

Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuimarisha juhudi kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs.

Rais Kenyatta amesema hayo kwenye hotuba aliyotoa kwa njia ya video katika mkutano kuhusu malengo ya SDGs ulioitishwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, kando ya kikao cha 76 ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa, huku akiongeza kuwa Kenya imepata maendeleo makubwa kuelekea malengo hayo.

Rais huyo amesisitiza tena ahadi ya Kenya ya kufikia malengo hayo, huku akisema nchi yake itaendelea na juhudi katika suala hilo.

Ameeleza kuwa ingawa maambukizi ya COVID-19 yameleta changamoto kwa uchumi na jamii, Kenya imepata maendeleo kwenye sekta mbalimbali za malengo ya SDGs ikiwemo elimu, jinsia na mabadiliko ya tabianchi.