UM waipongeza Tanzania kwa kuhimiza amani ya kikanda
2021-09-22 09:00:04| CRI

Umoja wa Mataifa umeipongeza Tanzania kwa juhudi zake za kuhimiza amani katika eneo la mashariki na kusini mwa Afrika.

Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Zlatan Milisic, alisema katika sherehe ya kuadhimisha Siku ya Amani ya Kimataifa, kuwa Umoja wa Mataifa inaipongeza Tanzania kwa kuwa msingi wa amani na utulivu, na kuleta pamoja nchi mbalimbali na kuzisaidia kujenga amani.

Bw. Milisic alisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na washirika wote kusaidia serikali na watu wa Tanzania kulinda na kuhimiza amani.