Eneo la viwanda lililojengwa na China nchini Ethiopia laingiza dola milioni 114 kutoka usafirishaji nje wa barakoa
2021-09-22 08:52:52| CRI

Eneo la viwanda la Ethiopia la Hawassa lililojengwa na China limetangaza kuwa limepata dola za Kimarekani milioni 114 kutokana na uuzaji wa barakoa kwenye soko la kimataifa.

Shirika la Habari la Ethiopia (ENA) limemnukuu meneja mkuu wa eneo la viwanda la Hawassa Bw. Fitsum Ketema, akisema mapato yanatokana na usafirishaji wa barakoa hizo hasa kwenye masoko ya Marekani na Ulaya kwenye mwaka wa fedha unaomalizika hivi karibuni .

Amesema licha ya changamoto zilizosababishwa na janga la COVID-19, kampuni zinazofanya kazi ndani ya eneo la viwanda la Hawassa ziliweza kupunguza athari za kiuchumi za janga hilo, na kuweza kuendelea na uzalishaji na usafirishaji wa barakoa.

Hapo awali serikali ya Ethiopia ilisema ina mpango wa kuingiza karibu dola bilioni 1 za Kimarekani kwa mwaka, kutokana na shughuli za uzalishaji kwenye maeneo yake ya viwanda.