Nchi za Afrika zapata dozi zaidi ya milioni 181 za chanjo ya COVID-19
2021-09-24 09:32:47| CRI

Nchi za Afrika zapata dozi zaidi ya milioni 181 za chanjo ya COVID-19_fororder_VCG111347766325

Kwa mujibu wa Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika (Africa CDC), nchi za Afrika zimepata dozi milioni 181.2 za chanjo ya COVID-19 hadi hivi karibuni na dozi milioni 136.3 tayari zimeshapokelewa na umma, ambapo asilimia 4.06 ya waafrika wamepewa dozi kamili za chanjo.

Nchi tano Morocco, Afrika Kusini, Misri, Algeria naTunisia zimekuwa nchi zinazopata na kutoa chanjo kwa wingi zaidi kwa raia wao. Nchini Morocco, kiwango cha utoaji wa chanjo kimefikia asilimia 48.63.

Kituo hicho pia kimesema hadi sasa vipimo visivyopungua 70,739,842 vya virusi vya Corona vimefanyika katika nchi za Afrika.