Makamu wa rais wa Zimbabwe asema kauli za kupotosha na habari feki hazitaharibu urafiki kati ya China na Zimbabwe
2021-09-27 14:26:49| cri

Gazeti la “The Herald” la Zimbabwe tarehe 24 lilitoa makala iitwayo “Hatutakuwa kibaraka wa Marekani katika kuipinga China”, ambayo inalaani kitendo cha Marekani cha kukashifu makampuni ya China nchini Zimbabwe, ili kuwaamsha wanahabari na watu wa Zimbabwe wasidanganywe na kutumiwa na Marekani.

Makamu wa rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga ambaye ni waziri wa afya wa Zimbawe jana alisema China na Zimbabwe ni wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili. Hivi karibuni kumekuwa na kauli za kupotosha ili kuharibu urafiki na ushirikiano kati ya nchi mbili, lakini kauli hizo zisizo sahihi na habari feki hazitaharibu uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Zimbabwe.