China yapeleka kikundi kipya cha manowari katika Ghuba ya Aden kwa ajili ya jukumu la usindikizaji
2021-09-27 08:52:48| CRI

China yapeleka kikundi kipya cha manowari katika Ghuba ya Aden kwa ajili ya jukumu la usindikizaji_fororder_VCG111300130548

Kikundi kipya cha 39 cha manowari za Jeshi la Majini la Ukombozi wa Watu wa China limeondoka mjini Qingdao, mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, jana Jumapili kuelekea kwenye Ghuba ya Aden na bahari ya Somalia ambapo kitatekeleza jukumu la usindikizaji.

Katika kujiandaa na jukumu hilo, manowari hizo zilifanya mazoezi ya matumizi ya silaha, kupambana na ugaidi na uharamia, na pia jinsi ya kuongeza mahitaji wanapokuwa baharini.

Jeshi la Majini la China lilianza kutekeleza majukumu ya usindikizaji katika Ghuba ya Aden na bahari ya Somalia mwezi Desemba mwaka 2008.