Mkutano wa pili wa usafirishaji endelevu duniani wafungwa
2021-10-18 08:39:36| CRI

Mkutano wa pili wa usafirishaji endelevu duniani wafungwa_fororder___172.100.100.3_temp_9500027_1_9500027_1_1_c1b03f5a-88df-4f61-a509-c9239eeb36fe

Mkutano wa pili wa usafirishaji endelevu duniani wa Umoja wa Mataifa umefungwa mjini Beijing.

Mkutano huo ulijadili mada mbalimbali zikiwemo maisha ya watu, maendeleo kwa njia isiyoleta uchafuzi, maendeleo yenye usalama, juhudi za kukabiliana na janga la COVID-19 na kufufua uchumi.

Mkutano huo umetoa wito wa kuharakisha kutimiza usafirishaji na uchukuzi endelevu ili kupunguza utoaji wa hewa zinazoongezeka joto kwa kiasi kikubwa, na kuboresha maisha ya mabilioni ya watu.

Pia mkutano huo umetoa Azimio la Beijing, ambalo linaeleza matumaini ya washiriki wa mkutano huo kuhusu maendeleo ya usafirishaji endelevu duniani katika siku zijazo, na kupendekeza kuchukua hatua za kujumuisha, kuhusisha sayansi mbalimbali na mashirika tofauti, ili kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika usafirishaji.