Bach aeleza imani yake kwa kufanikisha Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing
2021-10-19 08:27:33| CRI

Bach aeleza imani yake kwa kufanikisha Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing_fororder_VCG31N1347238200

Tochi ya Olimpiki imewashwa jana katika sehemu ya chimbuko la Michezo ya Olimpiki, nchini Ugiriki.

Mwenyekiti wa Kamati Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach, amesema kuwashwa na kupokezana Tochi ni muhimu zaidi kuliko Michezo ya Olimpiki na mashindano, pia ameeleza imani yake kuwa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing itafanikiwa.

Amesema, kazi ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing imefanyika vizuri, wameona ufanisi wa China wakati ikikabiliana na COVID-19, ujenzi wa majumba ya mashindano umekamilika miezi kadhaa iliyopita, na sasa mashindano ya majaribio pia yanafanyika kwa usalama.

Jumamosi, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ilifanya mkutano na wanahabari na kusifia mashindano ya majaribio yanayofanyika mjini Beijing, na kusema maoni ya wanamichezo wanaoshiriki kwenye mashindano ya majaribio ni mazuri.