Rais Xi Jinping wa China atoa wito wa kujenga nguvu ya China katika sayansi na teknolojia
2021-10-27 09:17:01| cri

Rais Xi Jinping wa China atoa wito wa kujenga nguvu ya China katika sayansi na teknolojia_fororder_习

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa wanasayansi na wanateknolojia nchini kuendelea kujitahidi kujenga nguvu za China katika sayansi na teknolojia.

Rais Xi amesema hayo alipotembelea maonyesho ya mafanikio ya China katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia katika kipindi cha Mpango wa 13 wa Miaka Mitano (2016-2020) mjini Beijing.

Rais Xi alibainisha kuwa China imepata maendeleo makubwa ya kisayansi na kiteknolojia katika kipindi hicho. Wakati China ikianza safari mpya ya kujenga nchi ya kijamaa ya kisasa katika nyanja zote, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia utakuwa na nafasi muhimu katika kukuza maendeleo ya jumla ya nchi.

Maonyesho hayo yameshirikisha zaidi ya vifaa na vielelezo 1,500. Miongoni mwao ni chombo cha uchunguzi wa mwezi cha Chang'e-5, kigari cha kuchunguza Mars, sampuli ya kompyuta ya quantum Jiuzhang, na nyambizi ya Fendouzhe.