Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja” lahimiza maendeleo ya Kenya
2021-11-25 08:53:07| CRI

Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja” lahimiza maendeleo ya Kenya_fororder_头图 肯尼亚

Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja” lililotolewa na China miaka minane iliyopita, limetoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Kenya.

Ripoti iliyotolewa na taasisi ya sera za Afrika, inasema tangu pendekezo hilo lilipotolewa mwaka 2013, China imefadhili miradi ya miundombinu ya kisasa kama reli, barabara, mabwawa, viwanda na mawasiliano ya kidigitali, ambavyo vimeongeza nguvu ya uhai kwenye ukuaji wa uchumi wa Kenya.

Akizungumza jana kwenye mkutano kuhusu ripoti hiyo Balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhou Pingjian ameipongeza serikali ya Kenya kwa maendeleo iliyopata kupitia ushirikiano huo.

Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Sera za Afrika Profesa Peter Kagwanja amesema kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwenye miradi ya Ushirikiano kati ya China na Kenya, nchi nyingine za Afrika zinaweza kuiga mfano huo.