China yazitaka baadhi ya nchi kutoa sauti ya haki kuhusu ushirikiano wa China na Afrika
2021-11-26 08:27:40| CRI

China yazitaka baadhi ya nchi sauti ya haki kuhusu ushirikiano wa China na Afrika_fororder_外交部 头图

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema watu wa Afrika ndio wenye haki ya kutoa maoni kuhusu ufanisi wa ushirikiano kati ya China na Afrika, na amezitaka baadhi ya nchi kutoa sauti ya haki kuhusu ushirikiano huo, kusikiliza maoni ya watu wa Afrika na kufanya mambo mazuri na halisi kwa ajili ya Afrika.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Jean-Yves Le Drian hivi karibuni alipohojiwa na vyombo vya habari vya Ufaransa alitoa lawama kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika.

Bw. Zhao Lijian amesema China imeshangazwa na lawama hizo zisizoendana na hali halisi. Amesema China ni rafiki mkubwa na wa muda mrefu kwa watu wa Afrika, na imeendelea kuwa mshirika mkubwa wa biashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo. Tangu Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC lilipoanzishwa, kampuni za China zimejenga au kukarabati reli zenye urefu wa kilomita elfu kumi, barabara zenye urefu wa kilomita laki moja, na kutoa nafasi za ajira zaidi ya milioni 4.5 barani Afrika. Hatua hizo zote zimeharakisha kidhahiri maendeleo ya Afrika, na kuboresha maisha ya watu wa huko, maendeleo ambayo yanakubaliwa na kupongezwa na nchi za Afrika. Kwa hivyo majaribio ya kuchafua ushirikiano huo hayatafanikiwa.