Kampuni ya Huawei na UNESCO watoa mwito kwa Kenya kulea watu wenye vipaji vya Tehama kuhimiza uchumi wa kidigitali
2021-11-26 08:44:45| CRI

Kampuni ya Huawei ya China na Shirika la Elimu na Sayansi la Umoja wa Mataifa UNESCO wametoa mwito kwa Kenya kuweka mpango wa kulea vipaji vya Tehama ili kuhimiza uchumi wa kidigitali.

Kampuni ya Huawei tawi la Kenya na UNESCO wamezindua ripoti kuhusu vipaji kwenye Tehama na uchumi wa kidigitali wa Kenya, na kuainisha pengo la ujuzi wa Tehama nchini Kenya na mahitaji yaliyopo katika sekta hiyo. Ripoti hiyo imeipongeza Kenya kwa kuboresha elimu, ushirikiano na kuunga mkono hatua za sekta binafsi kwenye sekta ya Tehama.

Mkuu wa Kampuni ya Huawei tawi la Kenya Bibi Fiona Pan, amesema Kenya ni miongoni mwa nchi chache za Afrika zilizo mstari wa mbele kwenye kunufaika na teknolojia za kidigitali kwenye ongezeko la uchumi.